32Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee.
33Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu,
34nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa, kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo.
35Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo;
36aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, nao wakajenga mji wangeweza kuishi.