34nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa, kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo.
35Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo;
36aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, nao wakajenga mji wangeweza kuishi.
37Walilima mashamba na kupanda mizabibu, nayo ikazaa matunda mengi,
38Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana, wala hakuruhusu mifugo yao kupungua.