2Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui,
3wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini.
4Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi.
5Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika.
6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.