22Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige.
24Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda.
25Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, wanionapo, hutikisa vichwa vyao.
26Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, niokoe sawasawa na upendo wako.