21Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako.
22Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige.
24Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda.
25Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, wanionapo, hutikisa vichwa vyao.