19Na iwe kama joho alilozungushiwa, kama mshipi aliofungiwa daima.
20Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya.
21Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako.
22Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige.