23Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige.
24Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda.
25Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, wanionapo, hutikisa vichwa vyao.
26Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, niokoe sawasawa na upendo wako.
27Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.