28Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, watakaposhambulia wataaibishwa, lakini mtumishi wako atashangilia.
29Washtaki wangu watavikwa fedheha, na kufunikwa na aibu kama joho.
30Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, katika umati mkubwa nitamsifu.
31Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.