10Niliamini, kwa hiyo nilisema, “Mimi nimeteseka sana.”
11Katika taabu yangu nilisema, “Wanadamu wote ni waongo.”
12Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea?
13Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana.
14Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote.