12Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea?
13Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana.
14Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote.
15Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa Bwana.
16Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu.