119Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako.
120Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako.
121Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu.
122Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee.
123Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.