118Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure.
119Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako.
120Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako.
121Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu.
122Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee.