122Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee.
123Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli.
124Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako.
125Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu ili niweze kuelewa sheria zako.
126Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa.