134Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako.
135Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako.
136Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
137Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi.
138Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu.