132Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.
133Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale.
134Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako.
135Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako.
136Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.