158Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako.
159Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.
160Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.
161Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.
162Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.