15Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.
16Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.
17Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako.
18Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.
19Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako.