33Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho.
34Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote.
35Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha.
36Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.
37Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.