38Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa.
39Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema.
40Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.
41Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,
42ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.