40Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.
41Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,
42ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.
43Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.
44Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele.