Zaburi 119

Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.

Psalm 119:75 (UKJV) I know, O LORD, that your judgments are right, and that you in faithfulness have afflicted me.

73Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

74Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

75Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.

76Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

77Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.