76Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
77Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.
78Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.
79Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako.
80Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.