79Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako.
80Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.
81Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.
82Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?”
83Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako.