87Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako.
88Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako.
89Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.
90Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu.
91Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.