93Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.
94Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.
95Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako.
96Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka.
97Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.