91Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.
92Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu.
93Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.
94Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.
95Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako.