Zaburi 126

Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.

Psalm 126:3 (UKJV) The LORD has done great things for us; whereof we are glad.

1Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto.

2Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Bwana amewatendea mambo makuu.”

3Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.

4Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu.

5Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.