1Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake.
2Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.
4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.