1Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana,
2ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
3Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.