6Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.
7Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake.
8Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.
9Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu: