Zaburi 142

Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego.

Psalm 142:3 (UKJV) When my spirit was overwhelmed within me, then you knew my path. In the way wherein I walked have they privately laid a snare for me.

1Namlilia Bwana kwa sauti, nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie.

2Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu.

3Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego.

4Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu.

5Ee Bwana, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.