Zaburi 144

Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie?

Psalm 144:3 (UKJV) LORD, what is man, that you take knowledge of him! or the son of man, that you make account of him!

1Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu, aifundishaye mikono yangu vita, na vidole vyangu kupigana.

2Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.

3Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie?

4Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita.

5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.