Zaburi 144

Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita.

Psalm 144:4 (UKJV) Man is like to vanity: his days are as a shadow that passes away.

2Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.

3Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie?

4Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita.

5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi.

6Peleka umeme uwatawanye adui, lenga mishale yako uwashinde.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.