4Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita.
5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi.
6Peleka umeme uwatawanye adui, lenga mishale yako uwashinde.
7Nyoosha mkono wako kutoka juu, nikomboe na kuniokoa kutoka maji makuu, kutoka mikononi mwa wageni
8ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.