15Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.
17Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
18Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
19Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.