Zaburi 19

Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

Psalm 19:11 (UKJV) Moreover by them is your servant warned: and in keeping of them there is great reward.

9Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki.

10Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

11Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

12Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.

13Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.