2Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.
3Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki.
4Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu. Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,
5linafanana na bwana arusi akitoka chumbani mwake, kama shujaa afurahiavyo kukamilisha kushindana kwake.
6Huchomoza upande mmoja wa mbingu, na kufanya mzunguko wake hadi upande mwingine. Hakuna kilichojificha joto lake.