10Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, toka tumboni mwa mama yangu umekuwa Mungu wangu.
11Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia.
12Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira.
13Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.
14Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu.