11Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia.
12Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira.
13Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.
14Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu.
15Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo.