16Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu.
17Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga.
18Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura.
19Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie.
20Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.