18Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura.
19Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie.
20Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.
21Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.
22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe.