19Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie.
20Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.
21Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.
22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe.
23Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!