17Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu, licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa.
18Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,
19ili awaokoe na mauti, na kuwahifadhi wakati wa njaa.
20Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.