Zaburi 33

Maana neno la Bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo.

Psalm 33:4 (UKJV) For the word of the LORD is right; and all his works are done in truth.

2Msifuni Bwana kwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.

3Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.

4Maana neno la Bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo.

5Bwana hupenda uadilifu na haki; dunia imejaa upendo wake usiokoma.

6Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.