19Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
20huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.
21Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa.
22Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe.