17Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.
18Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.
19Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
20huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.
21Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa.