3Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu.
4Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika.
5Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.
6Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.
7Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu.