Zaburi 38

Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu.

Psalm 38:3 (UKJV) There is no soundness in my flesh because of yours anger; neither is there any rest in my bones because of my sin.

1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako.

2Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia.

3Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu.

4Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika.

5Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.