12Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.
13Umetufanya lawama kwa jirani zetu, dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka.
14Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, mataifa hutikisa vichwa vyao.
15Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele,
16kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.