22Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.
23Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele.
24Kwa nini unauficha uso wako na kusahau taabu na mateso yetu?
25Tumeshushwa hadi mavumbini, miili yetu imegandamana na ardhi.
26Inuka na utusaidie, utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.